Kiungo wa zamani wa Yanga,
Abdi Kassim ‘Babi’ sasa amekuwa lulu nchini Malaysia ambako anaichezea timu ya
Ligi Kuu Malaysia, University Technology Mara FC (UiTM).
Babi ambaye timu yake sasa
iko katika nafasi ya sita, tayari amezivutia kutoka nchini Bahrain na Korea
Kusini.
Mtanzania huyo ambaye ni
tegemeo katika kiungo cha UiTM amezivutia timu hizo na tayari zimewasiliana na
klabu yake kutaka kujua zaidi kuhusiana naye.
“Kweli wametuma maombi ya
kutaka watumie video zangu zaidi, pia profile kuhusiana na nilikocheza kabla ya
kuja hapa,” alisema Babi alipozungumza na SALEHJEMBE.
“Baada ya hapo, sijajua nini kitakachofuata lakini mimi nimekuwa nikiendelea kupambana vilivyo kuhakikisha timu yangu inafanya vizuri,” alisisitiza.
0 maoni:
Post a Comment