BAO
la utata la Mfaransa Bafetimbi Gomis limeipa Swansea City ushindi wa
1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu
Uwanja wa Emirates, London.
Bafetimbi
alifunga bao la dakika za lala salama kwa msaada wa teknolojia kwenye
mstari wa lango, hicho kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa The Gunners.
Arsenal
inabaki nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa pointi
zake 70 ilizovuna katika mechi 35, ikiwa nyuma ya Manchester City wenye
pointi 73 za mechi 36 na mabingwa, Chelsea wenye pointi 84 za mechi 36
pia.
Manchester United ni ya
nne kwa pointi zake 68 za mechi 36 wakati Liverpool yenye pointi 62 za
mechi 36 ni ya tano na Tottenham Hotspur yenye pointi 58 za mechi 36 ni
ya sita.
Swansea wanaopanda
nafasi ya nane sasa kwa kufikisha pointi 56 baada ya mechi 36,
wanazidiwa pointi moja tu na Southampton walio nafasi ya saba.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny,
Monreal, Coquelin/Wilshere dk60, Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez na
Giroud/Walcott.
Swansea;
Fabianski, Rangel/Richards dk60, Fernandez, Williams, Taylor, Cork,
Dyer/Barrow, Shelvey, Ki/Gomis, Montero na Sigurdsson.
0 maoni:
Post a Comment