Yanga imeongoza kwa kufunga mabao mengi msimu huu huku Simon Msuva akifunga mabao 17. Mabingwa wa Tanzania bara Dar Young Africans imefunga magoli 52 ambayo ni asilimia 15 ya mabao yote yaliyofungwa msimu huu.
kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi Jumla ya mabao 348 yamefungwa msimu huu na timu zote, wakati huo huo Ruvu shooting na Polisi Morogoro ndio timu zilizofunga magoli machache Zaidi kwa kufunga mabao 16 kila moja ambayo ni sawa na asilimia 5.
Hata hivyo magoli ya msimu huu yameshindwa kufikia magoli ya msimu wa mwaka jana ambapo magoli 401 yalifungwa na Yanga pekee ilishinda magoli 61.
0 maoni:
Post a Comment