May 13, 2015

SIKILIZA HII YA HANS POPPE KUHUSIANA NA KOPUNOVIC

HANS POPPE
Bosi wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Kocha Goran Kopunovic ana kila sababu ya kuchagua, abaki au aende.

Hans Poppe amesema mazungumzo yao na Kopunovic ametaka dau kubwa hadi Sh milioni 28 kwa mwezi kama mshahara.

“Kweli bado hatujaelewana katika suala la maslahi. Sisi tunataka aendelee kubaki, lakini kwa fedha anayotaka hatuwezi kutoa.

“Kwa mwezi wadhamini wanatupa shilingi milioni 30 kwa mwezi kulipa wachezaji mishahara, yeye anataka achukue yote milioni 28.

“Hivyo tumemuachia yeye aamue kwa fedha ambazo tumemuambia. Kama hataweza basi atakwenda,” alisema Hans Poppe.

Taarifa za ndani ya Simba zimeeleza, kocha huyo ametaka mshahara wake upande kutoka dola 5,000 hadi dola 14,000 kwa mwezi.


Hali ambayo imeifanya Simba ishindwe kutoa fedha hizo na kusisitiza ikishindikana basi wataendelea kutafuta makocha wengine.

0 maoni:

Post a Comment