Bilionea Aliko Dangote
Uongozi wa Ndanda FC unajipanga
kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili
ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu
ujao haujaanza.
Salehjembe ameripoti
kwamba mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na
udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga
kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya mikakati ya
kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu
ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi imemalizika
bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi
litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa
ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia
nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema
Omari.
Dangote, raia wa Nigeria, kwa
sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea,
anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni
2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya
England.
0 maoni:
Post a Comment