MSHAMBULIAJI
wa zamani wa kimataifa wa Bulgaria, Dimitar Berbatov anatafuta timu ya
tatu ya kujiunga nayo England, baada ya kutemwa na AS Monaco ya
Ufaransa.
Berbatov
alijiunga na vigogo hao wa Ligue 1 Januari mwaka 2014 kutoka Fulham ya
England na atakumbukwa kwa kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-1
kwenye dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Pamoja
na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa yuko huru baada ya
kuachwa na Monaco, iliyomaliza katkka nafasi ya tatu kwenye Ligue 1
msimu huu.
Vigogo wa Ligue 1, AS Monaco wamethibitisha kumtema Dimitar Berbatov
Katika
taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim
Vasilyev, amesema; "Dimitar Berbatov ameonyesha kipaji chake chote na
soka babu kubwa. Dhahiri ni miongoni mwa washambuliaji wakubwa
waliojiunga na AS Monaco. Tunajivunia alicholeta katika klabu na tunamtakia kila la heri aendako,".'
Berbatov
alikuwa na wakati mzuri akichezea klabu ya Tottenham Hotspur kabla ya
kujiunga na Manchester United iliyomsaini kwa dau la Pauni Milioni
30.75 mwaka 2008.
Amefunga
mabao 48 katika Ligi Kuu ya England katika misimu minne chini ya kocha
Sir Alex Ferguson, kabla ya kuhamia Fulham, ambako alicheza kwa msimu
mmoja na nusu.
Mkongwe wa umri wa miaka 34 aling'ara Ligi Kuu England kabla ya kuhamia Ufaransa ambako nako ameacha kumbukumbu nzuri
0 maoni:
Post a Comment