Jun 2, 2015

MBEYA CITY YASAJILI 'STRAIKA'


Na Mwandishi Wetu, MBEYA
MSHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Ndanda FC ya Mtwara, Gideon Brown (pichani juu) amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na Mbeya City FC ya Mbeya.
Brown amechagua kujiunga na kikosi cha Juma Mwambusi katika msimu ujao huku akiweka kando ofa kadhaa, alizopata kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara alizopata hapo kabla.
Akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba huo mapema jana kwenye ofisi za MCC FC zilizopo jengo la Mkapa Hall mjini Mbeya, Brown alisema kuwa limekuwa jambo zuri kwake kujiunga na timu ambayo inaweza kumpa mafanikio nje na klabu zingine zilizozoeleka.
“Watu wengi wengi wanaamini kuwa huwezi kufanikiwa bila kupita kule, binafsi nahisi ni tofauti kwa sababu kipaji kinaweza kuonekana popote,imani yangu nitafanikiwa hapa, City ni timu nzuri na ina mipango ya  ya kweli, nataka kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na imani yangu sitawaangusha wale wote wenye mapenzi na timu hii, najaua nitakuwa chini ya mwalimu Mwambusi, huyu ni kocha ambaye siku zote nimekuwa na kiu ya kufanya nae kazi, hili limetimia sasa” alisema  mshambuliaji huyo.
Msimu uliopita Brown alikuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Ndanda Fc akicheza michezo  21 akiwa kwenye kikosi cha kwanza, na kuifungia timu hiyo ya Mtwara jumla ya mabao 5, awali mshambuliaji  huyu amewahi kukupiga kwenye timu za KMKM ya  Zanzibar na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu ya visiwani humo pia amecheza kwenye kikosi cha Rhino ya Tabora na Moro United.

0 maoni:

Post a Comment