Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (pichani juu) amesema kwamba ‘hawasajili bendera fuata upepo’, bali wanasajili kulingana na mahitaji ya timu yao.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Poppe amesema kwamba watu wanapenda kuona Simba SC inasajili wachezaji wanaovuma, lakini huo si mpango wa uongozi wa klabu.
“Sisi tuna kikosi kizuri ambacho kilimaliza msimu uliopita vizuri. Sasa tunachofanya ni kukiongezea nguvu kikosi kwa mujibu wa tathmini ya kitaalamu. Tunasajili mchezaji ambaye tunamuhitaji, siye anayevuma,”amesema.
Aidha, Poppe ambaye na Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba mkakati mzima na mpango wa usajili uko vizuri.
“Kila kitu kiko vizuri, tunafanya mambo yetu kimya kimya, hatushindani na mtu kusajili, tutakuja kushindana mpira uwanjani, hao wanaosajili wanaovuma, acha waendelee, sisi tunasajili kwa mujibu wa mahitaji yetu,”amesema.
Hadi sasa, tayari Simba SC imesajili wachezaji watano wapya, ambao ni kipa Abraham Mohammed kutoka JKU ya Zanzibar, mabeki Samih Haji Nuhu kutoka Azam FC, Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu na kiungo Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City.
Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wamesajili wachezaji wanne tu ambao ni kipa Benedicto Tinocco kutoka Kagera Sugar, beki Mwinyi Hajji Mngwali kutoka KMKM na washambuliaji Malimi Busungu wa JKT Mgambo na Deus Kaseke wa Mbeya City.

0 maoni:
Post a Comment