Jul 29, 2015

KAZIMOTO ALITAKAA KWENDA MISRI AKAAMUA KURUDI SIMBA


KAZIMOTO AKIWA QATAR...
Kiungo Mwinyi Kazimoto amejiunga tena na Simba akitokea Al Markhiya ya Qatar.


Mwinyi amerejea Simba baada ya kujiunga na Al Markhiya akitokea Msimbazi. 

Ameichezea timu hiyo ya daraja la pilim misimu miwili, lakini ikashindwa kupanda daraja.
AKISAINI KUREJEA SIMBA.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Al Markhiya ukaamua kubadili asilimia kubwa ya wachezaji ilionao ili kuleta mabadiliko iweze kupanda daraja. Fagio likamkumba Kazimoto, lakini alikuwa na bahati.

Kwani wakati mabadiliko yanafanyika, yeye tayari alikuwa amepata ofa ya kujiunga na Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu Misri.
HANS POPPE AKIPOKEA MKWANJA WA KUMUUZA KAZIMOTO NCHINI QATAR.

Licha ya juhudi za kutaka kiungo huyo ajiunge na Petrojet, yeye alisisitiza anataka kurejea nyumbani na mwisho, amejiunga na Simba!

"Ni kweli tumefanya juhudi kumshawishi kwamba Petrojet ingekuwa changamoto nzuri kwake. Lakini alikataa katakata na akasisitiza anataka kurejea nyumbani, hatukuwa na ujanja.

"Kibaya kwa wachezaji wa Tanzania, wengi wanataka kubaki Tanzania, ni waoga wa changamoto," kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya al Markhiya huko Qatar.

0 maoni:

Post a Comment