Oct 16, 2015

BOBAN ATAMBA SIMBA ITAFIA SOKOINE KESHO


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mbeya City inatarajiwa kuikaribisha Simba, kesho Jumamosi katika Ligi Kuu Bara lakini ujio wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ umeongeza nguvu kwenye kikosi cha Mbeya City ambapo amesema anaamini timu yake itaibuka na ushindi.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu
 yake hiyo, jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Boban alisema kwa 
jinsi alivyowaona wenzake katika muda mfupi, anaamini
 ushindi utapatikana.

“Hii imekuwa siku nzuri kwangu, nimegundua timu yetu ina
 kikosi bora, vijana wana vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza
 soka, binafsi hili limenishangaza na kunipa imani kuwa Simba
 hawana nafasi kwetu Jumamosi, tutawafunga,” alisema Boban.

Wakati huohuo, mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa 
kwenye Uwanja wa Sokoine, umesababisha kuwe na gumzo
 kubwa mkoani hapa, ambapo umekuwa ukizungumzwa katika
 vijiwe vingi vya soka.

Kutokana na hali hiyo, ulinzi ulikuwa mkali katika mazoezi ya Mbeya City ambayo ipo chini ya Kocha Meja Abdul Mingange.

0 maoni:

Post a Comment