OLUNGA (KULIA) AKISHANGILIA NA WENZAKE WA GOR MAHIA... |
Simba inapambana muda wote kuhakikisha
inamsajili straika Michael Olunga wa Gor Mahia, lakini nahodha wa Yanga, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ ni kama anataka kutibua dili hilo aliposema; “Huyo Olunga
hana lolote, isipokuwa ana bahati tu.”
Cannavaro alienda mbali kwa kusema, siku Yanga
ilipocheza na Gor Mahia ni kweli Olunga aliwasumbua na kufanikiwa kufunga bao
moja katika ushindi wa mabao 2-1 walioupata, lakini hana uwezo wa kusumbua
katika ligi.
CANNAVARO |
Cannavaro amesema: “Ujue siku ile tulipocheza
na Gor Mahia, Olunga alikuwa na bahati na kweli alitusumbua lakini sidhani kama
ana uwezo mkubwa kiasi cha kututisha.”
“Kwa kweli alibahatisha tu, nasikia Simba
wanataka kumsajili. Waache wamsajili halafu tukutane naye katika ligi (Ligi Kuu
Bara) ndipo watakapoona kama wanamsajili mchezaji wa kawaida tu.”
Cannavaro alisema anatamani wakutane tena na Gor Mahia katika mechi zijazo za Kombe la Kagame ili kuthibitisha kauli yake na kuwahakikishia Simba kwamba wanataka kusajili mchezaji wa kawaida.
0 maoni:
Post a Comment