Jul 16, 2015

KIBURI CHAMUONDOA VALDEZ MAN UNITED

Victor-Valdes-training
Hatimaye kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amefumbua kile kilichokua kimejificha baada ya kushuhudia golikipa Victor Valdez akiachwa katika safari ya ‘Pre-season’ nchini Marekani.

Akiongea kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari katika ‘tour’ hiyo ya nchini Marekani, pamoja na mambo mengine, Van Gaal alithibitisha kuwa klabu inajiandaa kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona.

Van Gaal akatoboa kwamba, Valdez aligoma kucheza katika mechi za U21 ikiwa ni utaratibu wa kujijenga kurudi katika fomu yako ya kawaida.

Van Gaal amesema, Valdez alienda kinyume na aliichoita ‘philosophy’ yake. Van Gaal huwamuru wachezaji kujiunga na timu ya vijana ya U21 katika hali ya kuwafanya warudishe fitness zao, lakini Valdez alikataa imefahamika.

Pamoja na sintofahamu ya golikipa David de Gea, lakini Van Gaal anasema hawawezi kumvumilia mchezaji kama Valdez na kumshangaa kwamba walimsaidia kurudi katika hali yake, ikiwa ni pamoja na kumpa mkataba lakini amekiuka masharti.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa De Gea, kocha huyo alisema ni upuuzi kuuliza swali hilo kwani De Gea anaonesha ‘commitment’ na ueledi mkubwa kikosini hapo.

Kuhusu DiMaria, Van Gaal alisema, mchezaji huyo ni mali yao lakini akasisitiza kuwa soka ni mchezo usiotabirika na kwamba mashabiki wasubiri kuona hadi mwisho itakuwaje.

Aidha katika mkutano huo na waandishi wa habari, wachezaji wapya walitambulishwa huku wakiulizwa pia maswali na waandishi katika utaratibu wa kawaida kabisa wa media.

Kwingineko tetesi zinasema kuwa Manchester United inamuwinda golikipa Romero wa timu ya taifa ya Argentina huku Real Madrid nao wakiingilia dili hilo.

0 maoni:

Post a Comment