Pamoja
na maandalizi ya kambi mjini Lushoto, Simba wametumia muda wao mchache
kutembelea kituo cha watoto yatima cha Irente.
Wakiongozwa
na Kocha Dylan Kerr, Simba na kikosi chao kizima walitua katika kituo hicho
kilichopo Lushoto pia na kuzungumza na watoto hao ikiwa ni pamoja na
kuwaliwaza.
Kerr
alionekana kufurahishwa na suala hilo na kusema lilikuwa jambo zuri.
“Kama
watu wanaoaminika au wanaotazamwa na jamii, ni jambo jema kuungana na wanajamii
wengine kama tulivyofanya,” alisema Kerr raia wa Uingereza.
0 maoni:
Post a Comment