Jul 5, 2015

NASRI AWACHIMBA MKWARA MZITO ARSENAL….


Nasri 2
Samir Nasri ametupilia mbali uvumi unaomhusisha na kumuomba Arsene Wenger kama kuna uwezekanao wa kurudi kukipiga tena Arsenal.
Kwa mujibu taarifa zilizoenea siku ya Alhamisi wiki iliyopita, inasemekana Nasri kwa sasa hajatulia katika klabu yake ya Man City, hivyo kuomba kurudi tena katika klabu yake hiyo ya zamani.
Lakini kupitia aakaunti yake ya Twitter, Nasri amekanusha vikali na kuandika hivi.
Nasri
Mwanzoni kabisa Nasri aliposti ujumbe huu hapo juu lakini ghafla aliufuta na kuandika ujumbe huu hapa chini.
‘Never ask anyone for a comeback so stop with those silly rumors [sic]’
Nasri then posted: ‘Never asked anyone to comeback!! Really happy where i am right now so stop with your silly story.’
Akiwa  anamaanisha hivi;
“Sijamuomba yeyote yule kurudi Arsenal, hivyo acheni uzushi usio na mantiki”.
“Ninafurahia maisha ya hapa nilipo, hivyo acheni habari zenu za kizushi”.
Ikumbukwe, Nasri aliondoka Arsenal mwaka 2011 na kujiunga na matajiri wa jiji la Manchester, timu ya Manchester City.

0 maoni:

Post a Comment