Jan 15, 2016

ALICHOSEMA KOCHA MPYA SIMBA NA ALICHOSEMA KOCHA MPYA COASTAL UNION

MAMBO mengine ukiyasikia unaweza
kucheka sana, yaani ni kama muvi
fulani ya kichekesho. Jackson Mayanja
alikuwa Kocha wa Coastal Union mpaka
juzi kati, lakini sasa ametua Simba.
Coastal wakamchukua Ally Jangalu
kuziba nafasi yake.
Mayanja kwenye mazoezi yake ya
kwanza kabisa alipowaangalia wachezaji
wa Simba akashika mdomo. Akashangaa
na kujisemea: “Mbona hawa wachezaji
hawako fiti kabisa? Hapa nina kazi
ngumu kwelikweli ya kufanya.”
Alienda mbali zaidi kwa kusema
kwamba wasingefanya lolote msimu
huu.
Sikia sasa. Jangalu akatoa naye ya
mwaka akamwambia: “Mbona hii
Coastal uliyoiacha ndiyo iko unga
zaidi?”

Jangalu amesema anachokifanyia kazi
kikosini humo kwa sasa ni kukijengea
ukakamavu, kwani anasema kikosi
kilikuwa hakina mwelekeo.
“Nimewakuta wachezaji hawana fitinesi,
hawana pumzi na hilo ndilo
ninalopambana nalo kwa sasa, naamini
watarejea kwenye ligi na kasi kubwa
tofauti na walivyoanza,” alisema.
Jangalu ambaye amepokea mikoba ya
Mganda Mayanja aliongeza: “Coastal
itakuwa timu yenye mfano hapa Tanga,
nimejipanga kuiweka kwenye ushindani
mkali.”
Alisema tayari ameishaona wachezaji
wameanza kurejea kwenye ari ya
kujituma na hilo ndilo inalompa
matumaini.
“Wachezaji wameanza kurejea kwenye
mstari na wapinzani wajiandae kwa
upinzani si kama walivyokuwa
wamezoea kuwa ni daraja la kupatia
pointi,” alisema.

0 maoni:

Post a Comment