MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kati ya vinara, Azam
FC na African Sports ya Tanga
itachezwa kuanzia Saa 1:00 usiku
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Leo kutakuwa na jumla ya mechi tatu
za Ligi Kuu, Dar es Salaam, moja
Uwanja wa Karume kati ya JKT Ruvu
na JKT Mgambo na nyingine Uwanja
wa Taifa, kati ya Simba SC na Mtibwa
Sugar.
Na ili kuwapa fursa watu kuona mechi
zote mbili kubwa za leo kupitia Azam
TV, ndiyo maana mchezo mmoja wa
Dar es Salaam umepelekwa usiku.
Ikumbukwe Azam FC iliyo kileleni
mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 35
baada ya kucheza mechi 13,
ikifuatiwa na mabingwa watetezi,
Yanga SC wenye pointi 33 za mechi
13 pia, imepania kushinda mechi hiyo
ili kuzidi kupiga kasi katika mbio za
ubingwa.
Baada tu ya kutolewa katika Kombe
la Mapinduzi visiwani Zanzibar wiki
iliyopita, Azam FC ilirejea Dar es
Salaam mapema kuanza maandalizi
ya mechi dhidi ya Sports.
Na katika kipindi hiki kifupi
wamefanya hadi mazoezi ya ufukweni
kuhakikisha wachezaji wake
wanakuwa fiti kikamilifu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni
baina ya mabingwa wa zamani wa ligi
hiyo, Simba SC na Mtibwa Sugar
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia Saa 10:00 jioni.
Mabingwa hao wa zamani wa Ligi
Kuu, wanakutana Jumamosi ya leo
ikiwa ni wiki moja tangu wakutane
katika Nusu Fainali ya Kombe la
Mapinduzi visiwani Zanzibar, Mtibwa
Sugar ikiilaza Simba SC 1-0, bao
pekee la Ibrahim Rajab ‘Jeba’.
Na baada ya kipigo hicho, Simba SC
iliwafukuza makocha wake,
Muingereza, Dylan Kerr na Mkenya
Iddi Salim na sasa Mganda, Jackson
Mayanja ndiye yupo na timu.
Mtibwa Sugar nao wataingia katika
mchezo wa kesho wakiwa na
kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-1
na URA ya Uganda katika fainali ya
Kombe la Mapinduzi Jumatano.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati
ya JKT Ruvu na Mgambo JKT Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam, Toto
Africans na Prisons Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza, Stand United na
Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Mbeya City na Mwadui FC
Uwanja wa Sokoine, Mbeya na
Coastal Union na Majimaji wa Uwanja
wa Majimaji, Songea.
Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi
moja tu, mabingwa watetezi, Yanga
SCwakiikaribisha Ndanda FC Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC nayo inarejea kwenye Ligi
Kuu baada ya kutolewa katika Nusu
Fainali ya Kombe la Mapinduzi,
wakifungwa kwa penalti 4-3 na URA
kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika
90.
0 maoni:
Post a Comment