Apr 12, 2016

AZAM YAMZUIA FARID NA HIMID MAO KWENDA ULAYA SABABU IPO HAPA

Na Haji balou
UONGOZI wa Azam FC umezuia safari ya kiungo wake Farid Mussa  kwenda Ubelgiji kwa majaribio
ya kucheza soka ya kulipwa hadi
amalize mchezo wa marudiano wa
hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia Aprili 19.

Awali, makubaliano kati ya wakala wa Farid na Azam ilikuwa ni mchezaji huyo aondoke baada ya mchezo wa kwanza na Esperance uliofanyika Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Farid alifunga bao moja na kuseti
moja katika ushindi wa 2-1 na baada
ya hapo, benchi la Ufundi chini ya
kocha Muingereza, Stewart Hall
limeona linamuhitaji kinda huyo kwa
mchezo wa marudiano.

Mbali na Farid, kiungo Himid Mao pia
anatarajiwa kwenda Denmark kwenda kujaribu bahati yake.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad
Kawemba, amesema kwamba
wameiomba klabu inayomtaka Farid
kwa majaribio imsubiri kwa wiki moja
zaidi.

“Awali Farid Mussa alitakiwa
kuondoka mara moja kwa ajili ya
majaribio hayo, lakini tumewaomba
wenzetu wanaomtaka wamuache hadi amalizie mechi yetu ya pili dhidi ya Esperance na wamekubali, hivyo Farid ataondoka baada ya mechi hiyo,” alisema.

0 maoni:

Post a Comment