Na Haji balou
Mwamuzi wa mechi kali ya Jumatano yenye
ushindani mkubwa sana Ligi ya Mabingwa Uefa, ameteuliwa, ni yule aliyechezesha fainali Kombe la Dunia 2014 Mwamuzi wa Kiitaliano Nicola Rizzoli amepangwa na UEFA kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa baina ya Atlético Madrid na Barcelona katika uwanja wa Vicente Calderón timu hizo zikiwa zinawania kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Hii itakuwa mechi ya saba kwa Rizzoli kuchezesha Ligi ya Mabingwa katika toleo la 2015/16.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 44 anatambulika kwa ubora wake katika kazi yake, si bora tu, ni zaidi ya bora katika ulimwengu wa soka la leo.
Akiwa na uzoefu wa miaka 14 katika Serie A na FIFA tangu 2007, Rizzoli amejizolea sifa kubwa kwa kutenda haki na uwezo wa kuchezesha mechi kubwa.
Kwa mfano, Muitaliano huyo ndiye
aliyepuliza kipyenga fainali ya Kombe la Dunia 2014 Ujerumani dhidi ya Argentina.
Barca na Atlético zina historia ya mechi zilizochezeshwa na Rizzoli. Alikuwa mwamuzi Atletico iliposhinda 2-0 hatua ya makundi dhidi ya Olympiakos dimbani Calderón, hali kadhalia
Atletico iliposhinda 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen msimu uliopita raundi ya 16.
0 maoni:
Post a Comment