Na Haji balou
YANGA SC itamenyana na Coastal
Union katika Nusu Fainali ya
michuano ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), maarufu kama
Kombe la Azam Sports Federations
Cup 2016.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa
Mkwakwani mjini Tanga Aprili 24,
mwaka huu, siku ambayo Azam FC
itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Tanga Aprili 24,
mwaka huu pia.
Hiyo inafuatia droo iliyopangwa leo
studio za Azam TV, wadhamini wa
michuano hiyo, Tabata, Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya
taifa ya wanawake, Twiga Stars,
Esther Chabruma ndiye aliyechagua
timu za kumenyana katika Nusu
Fainali katika droo hiyo, akisimamiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
Coastal Union iliingia Nusu Fainali
baada ya kuitoa Simba SC kwa
kuifunga mabao 2-1, wakati Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1,
Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa
kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga
Ndanda FC 2-1.
Bingwa wa Kombe la ASFC, michuano iliyoanza na timu 64 Novemba mwaka jana, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Katika hatua ya awali, kila timu
ilipatiwa fedha za usafiri Sh Milioni 3,
na vifaa vya mashindano kutoka kwa
wadhamini, Azam TV ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Bilioni 3.3.
Bingwa wa Kombe la ASFC
atajinyakuliwa kitita cha Sh. Milioni
50, Fainali inatarajiwa kuchezwa wiki
moja baada ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kumalizika.
Mara ya mwisho michuano hiyo
ilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu
ikaifunga Baker Rangers ya
Magomeni katika fainali, wakati
ikijulikana kama Kombe la FAT
(Chama cha Soka Tanzania).
0 maoni:
Post a Comment