Apr 17, 2016

SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1UGENINI

Na Haji balou
NYOTA ya Nahodha wa Tanzania,
Mbwana Samatta imeendelea
kung’ara Ulaya baada ya leo kuifungia tena klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya
Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa
Regenboogstadion mjini Waregem,
Samatta alifunga bao la kwanza
dakika ya saba tu kwa kichwa
akimalizia kona ya mkongwe wa umri wa miaka 25, Mbelgiji Thomas Buffel.

Beki wa Kongo mzaliwa wa Ufaransa, Marvin Baudry akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 15 kuipatia Genk bao la pili, kabla ya
mshambuliaji Msenegali, M'Baye Leye kuifungia SV Zulte-Waregem bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.

Hilo linakuwa bao la nne kwa Samatta katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.

0 maoni:

Post a Comment