May 24, 2016

YANGA KUPAMBANA NA TP MAZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Haji balou
YANGA SC imepangwa kundi la A
katika Kombe la Shirikisho Afrika
pamoja na mabingw awa zamani
barani, TP Mazembe ya DRC, MO
Bejaia ya Algeria na Medeama ya
Ghana.

Kundi B linaundwa na timu za
Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni  mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za  Morocco.

Mechi za mzunguko wa kwanza
zitachezwa Juni 17, mwaka huu na
Ratiba hiyo inamaanisha Yanga
itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC.

0 maoni:

Post a Comment