Kapombe (kushoto) siku walipocheza na Simba
MCHEZAJI kiraka wa Azam fc,
Shomari Salum Kapombe amesema matokeo mabaya wanayopata Prisons ndio
chanzo cha kuwakazia jana usiku katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara
iliyomalizika kwa suluhu uwanja wa Azam Complex.
“Prisons walifungwa mechi
iliyopita na Yanga, leo wamekuja na nguvu. Wameonesha kiwango kizuri na
nidhamu ya mchezo. Wamejilinda vizuri na kucheza mpira”.
“Tumejitahidi kufika mara nyingi golini kwao, lakini kipa wao (Mohammed Yusuph) amekuwa imara”.
Kwa matokeo ya jana, Azam fc
wanaendelea kushika nafasi ya pili kwa pointi 27 baada ya kushuka
dimbani mara 15, wakati Yanga wanaongoza msimamo kwa pointi 31 baada ya
kucheza mechi 15.
Kapombe amesema baada ya mechi
hiyo, sasa wanaelekea macho yao katika mechi ya marudiano ya ligi ya
mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merreick.
Mechi ya kwanza Azam
walishinda 2-0 na mechi ya marudiano itayopigwa mwishoni mwa wiki hii,
matajiri wa Dar wanahitaji ushindi au kufungwa magoli yasiyozidi mawili.
0 maoni:
Post a Comment