Feb 23, 2015

LUIS NANI APIGA BONGE LA BAO KISHA AANGUSHA KILIO UWANJANI

 Kiungo wa Man United anayecheza Sporting Lisbon kwa mkopo amefunga bonge la bao, halafu akaanza kulia.


Nani amefunga bao hilo umbali wa zaidi ya mita 30 wakati Sporting ilipishinda Gil Vicente kwa mabao 2-0, jana.
 
Baada ya kufunga bao hilo safi kabisa, Nani alijilaza na kuanza kulia.
Licha ya wenzake kumshawishi kuinuka, aliendelea kulia huku akiinua mikono juu akionyesha kumshukuru Mwenyezi Mungu.
 
Nani ,28, alipelekwa kwa mkopo katika timu yake hiyo iliyomkuza kisoka baada ya kuonekana hana kiwango kizuri.
Wakati wa Alex Ferguson na Man United ikiwa tishio, Nani alikuwa mmoja wa wachezaji bora wanaotegemewa.




0 maoni:

Post a Comment