Kiungo wa
zamani wa Simba, Pierre Kwizera ameanza vibaya katika kikosi chake kipya nchini
Rwanda.
Rayon Sports,
imekumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa watani wao wa jadi APR katika
mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali, juzi.
Kwizera ambaye
alicheza katika mechi hiyo na kuonyesha kiwango kizuri.
Lakini mambo
yakawa magumu kwao katika kipindi cha pili kwani APR walifunga mabao yote ndani
ya hizo dakika 45 za pili.
Mabao ya APR
yalifungwa na Nsahindula Michelle, emiry Bayisenge, Yannick Mukunzi na Sekamana
Maxime.
0 maoni:
Post a Comment