NAHODHA
wa kikosi cha Italia kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini
Ujerumani, Fabio Cannavaro amehukumiwa kifungo cha miezi 10 jela kwa
kukiuka amri ya kutofika katika nyumba yake iliyozuiliwa na Mamlaka.
Cannavaro
mwenye umri wa miaka 41, amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za kukwepa
kodi na Oktoba Mamlaka mjini Naples ilizuia mali za karibu Pauni 732,737
zinazohusishwa na mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus
pamoja na mkewe.
Kaka
wa Cannavaro, Paolo mwenye umri wa miaka 33, ambaye anachezea timu ya
Ligi Kuu Italia, Sassuolo, naye amehukumiwa kifungo cha miezi sita na
mkewe Daniela Arenoso mwenye umri wa miaka 40 miezi minne.
Watatu hao wamekata rufaa na kifungo chao kimesitishwa hadi mwisho wa rufaa yao.
Cannavaro amehukumiwa miezi 10 jela, ingawa kifungo chake kimesitishwa kupisha rufaa yake
Ndugu hao akina Cannavaro na Arenoso waliponzwa na kwenda kutembelea nyumba hiyo wakati ipo kizuizini.
Cannavaro
alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or mwaka 2006 baada
ya kuiongoza Italia kutwaa Kombe la Dunia. Akahamia Real Madrid baada
ya hapo, ambako alikwenda kutwaa mataji mawili ya La Liga na vigogo hao
wa Hispania.
Beki wa
klabu ya Yanga SC ya Tanzania, Nadir Haroub Ali, amepewa jina la utani
Cannavaro kutokana na Mtaliano huyo aliyeichezea mechi 136 Azzuri.
0 maoni:
Post a Comment