Feb 26, 2015

AZAM TV ‘KURUSHA LIVE’ MECHI YANGA NA BDF BOTSWANA KESHO



Rhys Torrington (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Azam Media Group Limited, Yussuf Bakhresa (kushoto)
TELEVISHENI ya kisasa ya kulipia kwa gharama nafuu, Azam TV itaonyesha moja kwa moja mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya wenyeji BDF XI na Yanga SC ya Tanzania.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Lobatse mjini Lobatse, kuanzia Saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika za Mashariki utaonyeshwa moja kwa moja na Azam Two.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Muingereza Rhys Torrington ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, mipango yote ya kuonyesha mchezo huo imekamilika.
“Kila kitu kimekamilika na tunayo furaha kuwaambia wateja wetu kwamba kesho tutakuwa na zawadi nzuri kwao, ambayo ni mchezo wa Yanga na BDF XI, watautazama kupitia Azam TV,” alisema Torrington.
Katika mchezo huo wa kesho, Yanga SC inahitaji hata sare ili kuweza kusonga mbele, baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment