LIVERPOOL imetupwa nje ya michuano ya Europa League, baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na Besiktas kufuatia sare ya jula ya 1-1.
Tolgay
Arslan alitokea benchi na kuifungia Besiktas bao dakika ya 72 Uwanja wa
Ataturk, Istanbul nchini Uturuki akimalizia ‘pande’ la Demba Ba na
kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya Liverpool kushinda 1-0 katika
mchezo wa kwanza England.
Ba angeweza kufunga bao la ushindi dakika ya 92, kama asingegongesha mwamba akiwa umbali wa mita sita.
Baada
ya dakika 120, penalti za Besiktas zilifungwa na Ba, Lambert, Tore,
Lallana na Kavlak, wakati zilifungwa na Can, Hutchinson, Allen na Arslan
huku Lovren akikosa.
Kikosi
cha Besiktas kilikuwa; Gonen, Opare, Franco, Uysal, Kurtulus,
Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa/Arslan dk61, Sahan/Frei dk105 na Ba.
Liverpool:
Mignolet, Toure, Lovren, Skrtel, Moreno, Can, Allen, Sterling,
Ibe/Manquillo dk76, Sturridge/Lambert dk106 na Balotelli/Lallana dk82.
Wachezaji wa Liverpool wakisitika baada ya kutolewa Europa League na Besiktas, kulia Demba Ba akishangilia
0 maoni:
Post a Comment