BAADA ya kuwa
nje kwa majeruhi muda mrefu, kiungo mshambuliji wa Mbeya City Fc, Alex
Seth ‘Messi’ amerejea kikosini tayari kuendeleza mapambano katika
kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Seth amekaririwa na Tovuti ya
Mbeya City fc akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona majereha
yaliyokuwa yanamsumbua kwa kipindi kirefu na kumfanya kuikosa ligi kwa
kipindi kirefu.
“Nashukuru nimepona,nilikosa
ligi kwa kipindi kirefu mara ya mwisho nilicheza dhidi ya Tanzania
Prison msimu uliopita,narudi kuongeza nguvu kwenye kikosi, kama timu
tulikuwa na wikiendi mbaya baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga
lakini jumamosi hii naimani itakuwa ni sehemu nyingine ya furaha
kwetu hasa kwa kuongeza pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting”
alisema.
Akiendelea zaidi Seth alisema,
hivi sasa kwenye kikosi imani ya kila mchezaji ni kucheza kwa nguvu ili
kutafuta matokeo kwenye mchezo ujao huku akiamini kuwa hilo linawezekana
hasa ukizingatia morali iliyopo hivi sasa miongoni mwa nyota wa City
bila kujali nini kilikuwepo juma lililopita.
“Naomba mashabiki wawe na timu
yao, bado iko vizuri na kwa uwezo wa mwenyezi mungu naimani tutashinda
jumamosi, tunajua walikosa furaha baada ya mchezo uliopita lakini huu ni
wakati wao na waamini kwenye soka inawezekana kushinda mchezo
unaofuata hata kama ulipoteza mchezo uliopita” alimaliza.
0 maoni:
Post a Comment