Kama wewe ni shabiki wa muziki wa Africa
unaweza kuwa na hamu ya kufahamu ni single gani ambayo iko juu kwenye
chati za muziki huu duniani…. kwa sababu kazi yangu ni kukusogezea zote
muhimu, nakusogezea na hii kwamba video ya ‘Nitampata wapi’ ya Diamond
Platnumz kupitia kituo cha TraceTV ya Ufaransa imeicheza video hiyo kama
namba 1.
Mbali na video hiyo kuchezwa kama namba 1
kwenye kituo hicho cha Trace TV, Diamond Platnumz ana sababu nyingine
ya kufurahi mafanikio ya kuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kupitia video
yake ‘Nitampata wapi’ kufikisha views milioni 2 tangu iwekwe Nov 20,
2014.
0 maoni:
Post a Comment