MABINGWA watetezi wa ligi kuu
soka Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya ligi ya
mabingwa Afrika, Azam fc wanaendelea kujifua nchini Sudan kuelekea mechi
ya marudiano dhidi ya wenyeji Al Merrick itayopigwa kesho jumamosi
usiku uwanja wa Odmarman, mjini Khartoum.
Azam fc wataingia katika mechi ya kesho wakiwa na faida ya mabao
2-0 waliyovuna februari 15 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Dar es
salaam.
Mabao hayo yalifungwa na Didier Kavumbagu na Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
Licha ya kufanyiwa fitina za hapa na pale, kocha mkuu wa Azam,
Mcameroon, Joseph Marius Omog ameendelea na programu yake ya mazoezi
leo.
Azam wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kufungwa si zaidi ya goli 1-0 ili kusonga mbele.
0 maoni:
Post a Comment