Feb 27, 2015

MCHEZAJI SERBIA ATISHIWA KUUAWA KWA BUNDUKI KISA KUKOSA PENALTI

MCHEZAJI wa klabu ya Ligi Kuu ya Serbia, Novi Pazar ametishiwa kupigwa bastola na mashabiki baada ya kukosa penalti, taarifa ya chama cha Umoja wa Wachezaji Duniani, FIFPro imesema jana.
Ikiliita tukio hilo kama sheria mpya katika soka ya Serbia, FIFPro imesema kwamba mchezaji wa Novi Pazar, Zarko Udovicic alipaisha mkwaju wake wa penalti juu ya lango dakika ya 85 Jumamosi iliyopita katika mchezo dhidi ya FK Rad.
Siku mbili baadaye, mashabiki kadhaa wenye hasira walivamia chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji na kwenda kumuonyeshea mtutu wa bunduki usoni Udovicic, imesema taarifa ya FIFPro. Baada ya hapo, mchezaji huyo ameondoka kwenye klabu hiyo.
Zarko Udovicic has left Serbian club Novi Pazar after  fans threatened him with a gun for missing a penalty
Zarko Udovicic ameondoka Novi Pazar ya Serbia baada ya kutishiwa mtutu wa bunduki kwa kukosa penalti

Mirko Poledica, Rais wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa Serbia, Nezavisnost, amesema hakuna aliyechukua hatua baada ya tukio hilo kati ya Chama cha Soka Serbia au bodi ya Ligi.
"Nchini Serbia, hakuna shabiki aliyewahi kuchunguzwa au kutiwa hatiani baada ya kuwafanyia fujo wachezaji. Ndiyo maana wachezaji wanaogopa. Kila siku wanaishi kwa matumaini ifike wakati wasiwe na mashaka ya kugongewa milango na kupigwa na mashabiki, au kuchomewa moto gari zao,".
FIFPro imesema; "Kama ilivyo kwa mfanyakazi yeyote kitaaluma, kila mchezaji anastahili kuwekewa mazingira salama ya kufanyia kazi. Ni juu ya mamlaka za soka kuweka mazingira hayo salama,".
Udovicic had missed a penalty for Novi Pazar against FK Rad two days before the incident
Udovicic alivyopaisha penalty ya Novi Pazar dhidi ya FK Rad kabla ya kutishiwa mtutu wa bunduki siku mbili baadaye

0 maoni:

Post a Comment