Feb 26, 2015

JULIO AANZA MANENO COASTAL UNION

Na Oscar Assenga, TANGA
KOCHA Msaidizi wa Coastal Union, Jamhuri Kiwelu “Julio”amesema kuwa timu hiyo itapata matokeo mazuri katika mechi zake zilizosalia katika michuano ya Michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kutokana na ubora wa kikosi hicho
Julio alitoa wito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara kumalizika mazoezi ya timu hiyo ambapo alisema kuwa lengo la kujiunga na timu hiyo ni kuongeza nguvu ili kukiwezesha kikosi hicho kurudisha makali yake.
Jamhuri Kihwelo 'Julio' kushoto amesema Coastal Union itatisha

Alisema kuwa atahakikisha anatoa mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini.
“Mimi niliwahi kuifundisha Coastal Unionna kuiwezesha kupata mafanikio hivyo ni matumaini yangu kukiwezesha kikosi hichi kurejesha makali yake kwani timu hii ni kubwa na inaheshima yake kwenye soka “Alisema Kocha Julio.
Kocha huyo alisaini mkataba wa muda mfupi mpaka ligi kuu soka Tanzania mzunguko wa pili utakapomalizika ambapo atatumia nafasi hiyo kukipa makali kikosi hicho.
Alisema kuwa malengo makubwa yake ni kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara ikiwemo kuwataka wachezaji kushikamana na kuwa watulivu kila mechi ili kupata mafanikio.
Hata hivyo alisema kuwa hatasita kuwafukuza kwenye kikosi hicho wachezaji watakaokuwa watovu wa nidhamu na watakaojiona mastaa na kushindwa kuendana na kasi yake katika mazoezi.
“Nashukuru kutua Coastal Union sasa ni kazi tu tutahakikisha tunapambana kufa na kupona ili kuweza kupata matokeo mazuri kila mechi zilizosalia kwenye Ligi hiyo “alisema Julio.

0 maoni:

Post a Comment