Feb 8, 2015

KAGERA SUGAR YAFUTA MIKOSI IMESHINDA WENGINE WAPATA SARE

HATIMAYE Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza baada ya mechi nne za Uwanja wa nyumbani, kufuatia kuilaza 1-0 Mgambo Shooting Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jana.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Kagera wanacheza Uwanja wa Kambarage kama wa nyumbani, baada ya kuhama Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
 
Kagera ililazimika kuondoka Bukoba baada ya Uwanja wa Kaitaba kuanza kukarabatiwa Januari mwaka huu na kuhamia Kirumba, Mwanza.
Hata hivyo, baada ya kufungwa mechi tatu mfululizo Mwanza, uongozi wa timu hiyo ukadai unafanyiwa hujuma na wenyeji wa mkoa huo, Toto Africans hivyo wakahamia Shinyanga.
Atupele Green aliifungia Kagera jana 

Na jana bao pekee ka Atupele Green limewafanya wapate cha kuongea kuhusu Mwanza- kwamba kweli walikuwa wanafanyiwa fitina na wenye mji wao, Toto.
Kagera ilikuwa timu pekee iliyoibuka na ushindi katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana, baada ya mechi nyingine zote kumalizika kwa sare. 
 
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba SC ilitoka sare ya 0-0 na wenyeji Coastal Unin, Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mabingwa watetezi, Azam FC walitoka sare ya 2-2 na wenyeji Polisi, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, JKT Ruvu walitoka 1-1 na Mbeya City, Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Prisons walitoka 1-1 na Ruvu na Shooting, wakati Uwanja wa Nangwanda, Sijaona, Mtwara wenyeji Ndanda FC walilazimishwa sare ya 0-0 na Stand United ya Shinyanga.
 
Ligi hiyo inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Yanga SC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment