Mar 2, 2015

ARSENAL WAZINDUKA, WAICHAPA EVERTON 2-0

ARSENAL imezinduka kutoka kwenye kipigo cha Monaco Ligi ya Mabingwa, baada ya leo kuifunga mabao 2-0 Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Olivier Giroud alianza kufunga dakika ya 39 akimalizia pasi ya Mesut Ozil, kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili dakika ya 89.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aliwatema kikosini Per Mertesacker baada ya kipigo cha Monaco.
Matokeo hayo, yanaifanya Arsenal itimize pointi 51 baada ya kucheza mechi 27, nyuma ya Manchester City yenye pointi 55 za mechi 27 na Chelsea pointi 60 za mechi 26.
Kikodi cha Arsenal; Ospina, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Gibbs, Coquelin/Chambers dk89, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Rosicky dk82, Ozil, Alexis/Welbeck dk87 na Giroud.
Everton; Howard, Coleman, Jagielka, Stones, Garbutt, McCarthy, Besic/Naismith dk77, Barry/Gibson dk84, Mirallas/Lennon dk62, Barkley na Lukaku.
Giroud struggled in Arsenal's midweek defeat by Monaco but showed his delight at the Emirates after firing the Gunners in front
Giroud akishangilia baada ya kuifungia Arsenal leo

0 maoni:

Post a Comment