LIVERPOOL imeichapa mabao 2-1 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Anfield jioni ya leo.
Jordan
Henderson aliifungia bao la kwanza Liverpool dakika ya 11 kwa shuti la
umbali wa mita 20 baada ya kazi nzuri ya Steven Gerrard.
Edin
Dzeko akafanikiwa kuisawazishia Man Cty dakika 15 baadaye, kabla ya
Philippe Coutinho kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 75.
Kipigo hicho kinaifanya Man City ibaki na poitni zake 55 za mechi 27, wakati Liverpool imafikisha pointi 48 za mechi 27.
Kikosi
cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren,
Markovic/Sturridge dk76, Henderson, Allen, Moreno/KoloToure, Coutinho,
Sterling na Adam Lallana.
Man
City; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Nasri/Lampard dk83,
Toure, Fernandinho/Bony dk78), Silva, Aguero, Dzeko na Milner dk58.
Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuikfungia bao Liberpool leo
0 maoni:
Post a Comment