Rais wa Simba, Evans Aveva
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Rais wa Simba SC, Evans Aveva
amesema kuwa ana maelewano mazuri na Makamu wa Rais wa klabu hiyo,
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na kwamba hana ugomvi wowote na kiongozi huyo
wa wanamsimbazi.
Akizungumza katika mkutano mkuu
wa wanachama wa Simba SC uliofanyika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi
Oysterbay jijini hapa leo, Aveva amesema kuna taarifa zimekuwa
zikielezwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba hana uhusiano
mzuri na Kaburu, jambo ambalo amelikanusha vikali.
“Tumekuwa na matokeo mabovu na
mwenendo wa kusuasua katika timu yetu. Ni matokeo mabaya ikilinganishwa
na historia na jina la Simba Sports Club.
“Matokeo hayo yamekuwa yakiibua
maswali mengi huku baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza kuwa mimi
(Aveva) sina uhusiano mzuri na Kaburu.
“Ukweli ni kwamba mimi na
Kaburu tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, na si Kaburu tu, bali
viongozi wote wa Simba SC. Hizi taarifa kwamba ni ugomvi na Kaburu si
kweli,” amesema Kaburu.
Rais huyo pia ameeleza masuala
mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja,
kuongeza idadi ya wanachama kwa kuleta mtambo maalum wa klabu kwa ajili
ya kuchapisha kadi mpya za wanachama badala ya kuchapisha kwa watu
binafsi ili kupunguza gharama.
Ukawa hawarudishwi Simba
Aveva amesema kuwa kamwe
wanachama 72 waliofutiwa uanachama wa Simba SC hawatarudishwa kwa sababu
walifukuzwa kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo ya Msimbazi jijini hapa.
Aveva amesema kuwarudisha
kinyemela wanachama hao ni kukiuka misingi ya katiba kwani misingi ya
katiba hiyo ilifuatwa wakati wa kuwafutia uanachama.
0 maoni:
Post a Comment