Mar 13, 2015

HIVI ULIONA HANS POPPE ALIVYOWANANGA YANGA? CHEKI HII HAPA

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Han Poppe alitoa kali ya mwaka Jumapili mara tu baada ya watani, Simba na Yanga kumalizika.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Simba kushinda kwa bao 1-0 na kuwanyamazisha Yanga.
Lakini kama hiyo haikutossha baada Hans Poppe kusimama mbele ya mashabiki wa Yanga na kuanza kuwahoji kuhusiana na timu yao na mbwembwe nyingi walizokuwa nazo.
 
Hans Poppe aliwakumbusha Simba ilivyoonyesha kiwango hasa dakika za mwisho na kufunga bao bora kabisa.
Halafu baada ya hapo, aliondoka kama hile akiwaachia mkono kwa kusema “nendeni kule.”
Mashabiki wa Yanga walioonyesha kumcharua mtani wao huyo, walibaki kimyaa kwa kuwa ndiyo mpira ulikuwa umemalizika na wana machungu ya kufungwa.

0 maoni:

Post a Comment