Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba, kimeendelea kuitesa Yanga, hiyo ni baada ya jana
asubuhi kufanyika kikao kizito kati ya viongozi wote wa matawi wa Dar es Salaam
na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kisha kutolewa maoni ‘tata’.
Kikao
hicho, kilifanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga
kikiongozwa na Sanga na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ambacho wanachama
walidai uwepo wa wachezaji wasio na mapenzi, wakiwemo kutoka Simba, unaweza
kuwafanya wacheze bila kujituma.
Sanga amesema katika kikao hicho, viongozi hao wa matawi
wameuomba uongozi kufanya uboreshaji wa usajili wao msimu ujao baada ya kutokea
minong’ono mingi juu ya hujuma hizo.
“Leo
nimekutana na viongozi wa matawi na kujadiliana masuala mbalimbali ya timu,
likiwemo la kurejesha morali ya timu baada ya kufungwa na Simba.
“Pia
kuwataka kuungana kwa pamoja katika kuelekea mechi yetu na Platinum ya
Zimbabwe, hayo ndiyo ya msingi na kubwa zaidi viongozi wa matawi wameomba kuwepo
na uboreshaji katika mfumo wa usajili kwa kusajili wachezaji wenye moyo na
mapenzi na timu,” alisema Sanga.
Hivi
karibuni, kuliibuka maneno kuwa, kuna baadhi ya wachezaji ambao walitua klabuni
hapo wakitokea Simba, hawana moyo wa kujituma kama wengine, madai ambayo
uongozi wa Yanga umeyakanusha.
0 maoni:
Post a Comment