Kipa mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda amemtetea Barthez kwa kusema hastahili lawama kwa bao alilofungwa.
Ivo aliyewahi kudakia Yanga kwa zaidi ya misimu miwili amesema Barthez hastahili kulaumiwa kwa kuwa amefungwa bao bora.
“Bado
naamini Barthez ni kipa bora na mwenye uwezo wa juu, hatakiwi kulaumiwa
bali Okwi ndiye anatakiwa kupongezwa kwa kufunga bao kiufundi,” alisema
Ivo.
Barthez alifungwa bao pekee lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Jumapili iliyopita.
Okwi alifunga bao akiwa katika kasi kubwa na kupiga mpira wa juu uliompita kipa huyo akiwa ametoka kidogo nje ya lango.
0 maoni:
Post a Comment