Apr 8, 2015

AZAM FC WAUWEKA REHANI UBINGWA LIGI KUU, WALAZIMISHWA SARE 1-1 NA MBEYA CITRY

Frank Domayo wa Azam FC akifumua shuti katikati ya wachezaji wa Mbeya City leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
MABINGWA watetezi, Azam FC wamekwaa kisiki nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanawafanya Azam FC sasa wawe wanazidiwa pointi sita na vinara, Yanga SC wenye pointi 43 baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Coastal Union leo.
Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kipre Michael Balou dakika ya 61 kwa shuti la umbali wa zaidi ya mita 25.
Haikuchukua muda mrefu, Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Raphael Alpha kwa penalti dakika ya 64, kufuatia Erasto Nyoni kumuangusha Deus Kaseke.
Baafa ya hapo, timu hizo zilishambuliana kwa zamani na kipyenga cha mwisho, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao zaidi.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Serge Wawa, Mudathir Yahaya, Himid Mao, Kipre Bolou/Gaudence Mwaikimba dk80, Frank Domayo/Amri Kiemba dk56, John Bocco na Brian Majwega/Farid Mussa dk74.
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, Peter Richard, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso, Christian Sembuli, Kenny Ally, Deus Kaseke/Hamad Kibopile dk84, Paul Nonga/Peter Mapunda dk70, Raphael Alpha, Themi Felix na Peter Mwilanzi.

0 maoni:

Post a Comment