Philippe
Coutinho akishangilia baada ya kufunga bao pekee zikiwa zimesalia
dakika 20 mchezo kumalizika katika ushindi wa 1-0 wa Liverpool dhidi ya
Blackburn Rovers Uwanja wa Ewood Park, mchezo wa marudiano wa Robo
Fainali Kombe la FA. Mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bila
kufungana Uwanja wa Anfield mwezi uliopita. Liverpool sasa itamenyana na
Aston Villa katika Nusu Fainali Uwanja wa Wembley Jumapili ya Aprili
19.
0 maoni:
Post a Comment