May 4, 2015

PAC MAN: ILIBAKI KIDOGO TU NIJITOE PAMBANO NA MAYWEATHER

BONDIA Manny Pacquiao amesema kwamba alikaribia kujitoa katika pambano aliloliingiza dola za KImarekani Milioni 180 leo dhidi ya Floyd Mayweather, ambalo amepoteza kwa pointi.
PacMan amesema kwamba aliumia bega mazoezini na Kamisheni ya Michezo Nevada ilimkatalia ombi la kusogeza mbele pambano hilo la utajiri mkubwa zaidi kihistoria duniani.
Pacquiao aliamua kupanda ulingoni leo licha ya Kamisheni hiyo kukataa hata la kuchoma sindano ya ganzi katika chumba chake cha kuvalia kuzuia maumivu.
Manny Pacquiao revealed he had suffered an injury three weeks before the fight took place

Kamisheni pia ilikanusha kuwa na taarifa za mapema juu ya maumivu ya bondia huyo wa Ufilipino. 
Pacquiao amesema: "Maumivu yalirudi kwemnye raundi ya tatu na baada ya hapo sikuweza kutumia vizuri mkono wangu wa kulia,".
Kocha wake, Freddie Roach amesema: "Maumivu ya zamani ya bega hilo yalirudi kiasi cha wiki mbili na nusu kabla ya pambano. Yalivuruga mazoezi. Alifanyiwa vipimo (MRI), akapewa ruhusa ya matibabu, bega likaanza kupata nafuu siku hadi siku na tukaamua kupanda ulingoni,".
Mayweather addresses the media after taking his record to an unbeaten 48-0 against Pacquiao

Mayweather amejibu madai hayo ya mpinzani wake akisema; "Nilipata maumivu pia. Mikono yangu yote iliumia. Hizo ndiyo ngumi. Na kama angeshinda ningesema alikuwa bora katika usiku huo,".
Pacquiao amepoteza pambano kwa pointi mbele ya Maywether na hakupiga ngumi nyingi kama ilivyotarajiwa, ingawa mwenyewe awali alisema ni kwa sababu ya mpinzani wake kukimbia kimbia ulingoni.

0 maoni:

Post a Comment