May 4, 2015

TYSON: MAYWEATHER AMESHINDA KIHALALI

BINGWA wa zamani wa dunia uzito wa juu, Mike Tyson amemaliza ubishi kwa kusema Floyd Mayweather amemshinda kihalali Manny Pacquiao.
"Tumelisubiri kwa miaka mitano, nafikiri (Mayweather) ameshinda pambano, alimzidi ngumi Manny. Manny alikuwa ana mwanzo mzuri, lakini (Mayweather) akaimudu hiyo,"amesema Tyson.
"Alilimudu pambano, alikuwa ana nguvu (na) na amefanya kazi haswa," amesema.
"Ni zama zake, wakati wake. ni mtu babu kubwa sasa- hakuna mmoja anayeweza kusimama naye kwa wakati huu,"amesema. 
Former heavyweight world champion Mike Tyson at the MGM Grand on Saturday night to watch the fight

0 maoni:

Post a Comment