May 4, 2015

SAMATTA, ULIMWENGU ‘WAIPELEKA MBELE’ TP MAZEMBE LIGI YA MABINGWA

TANZANIA itaendelea kutajwa katika michuano ya Afrika licha ya timu zake zote kutolewa- kufuatia TP Mazembe kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa jioni ya leo kwa ushindi wa jumla wa 4-3 dhidi ya Stade Malien.
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu imeshinda mabao 2-1 leo Lubumbashi dhidi ya timu ya Mali. 
Mabao ya TP Mazembe yamefungwa na Jean Kasusula dakika ya 20 na Roger Claver Assale dakika ya 63.
Timu zote za Tanzania, KMKM, Polisi, Azam FC zimetolewa Raundi ya kwanza tu katika michuano ya Afrika.
Yanga SC ilijitutumua hadi raundi ya tatu kabla ya kutolewa jana na Etoile du Sahel ya Tunisia.

0 maoni:

Post a Comment