Feb 24, 2015

ALICHOSEMA KOCHA WA SIMBA BAADA YA KUFUNGWA NA STAND UNITED

Pamoja na kupoteza nafasi nyingi za kufunga, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kweli Ligi Kuu Bara ni ngumu.

Kopunovic amekubali hilo baada ya ile mechi waliyolala kwa bao 1-0 mjini Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United.


Ameiambia SALEHJEMBE kwamba kulikuwa na makosa mengi kwa mwamuzi, pia wachezaji wake kutotumia nafasi, lakini akasisitiza, ligi ni ngumu.

"Ukiangalia mechi utaona tulicheza vizuri tu, lakini kuna makosa kadhaa ya sisi kutotumia nafasi na hata mwamuzi hakuwa mzuri kwetu.

"Lakini bado naweza kusema ligi ni ngumu sana na ushindani uko juu. Kupoteza mechi hiyo na Stand, kweli imeniumiza.

"Najua hata wachezaji wameumia lakini ni suala la kuangalia mechi ipi inafuatia na nini cha kufanya," alisema Kopunovic.

0 maoni:

Post a Comment