Feb 24, 2015

YANGA SC YAMUACHA COUTINHO SAFARI YA BOTSWANA

Na Pince Akbarm DAR ES SALAAM
KIUNGO Andrey Coutinho raia wa Brazil hatakuwemo katika kikosi cha kikosi cha Yanga SC kinachoondoka kesho Dar es Salaam kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya BDF XI.
Yanga SC wanatarajiwa kuwa wageni wa BDF Ijumaa wiki hii katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Mbrazil huyo hayumo safarini kwa sababu ya majeruhi.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 na viongozi saba mjini Gaborone, tayari kwa mchezo ambao tayari wanaongoza kwa mabao 2-0.
Andrey Coutinho hatakwenda Botswana kwa sababu ni majeruhi 

Maana yake, Yanga SC wanatakiwa japo kulazimisha sare ugenini ili kutinga Raundi ya Kwanza ya michuano hiyo.
Katibu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema kikosi chao kitaondoka na wachezaji wote waliopitishwa na kocha wao Hans Pluijm.
Tibohora ambaye pia kitaaluma  ni kocha amesema kikosi chao kitaondoka na Ndege ya Shirika la Kenya tayari kwa mchezo huo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Ijumaa nchini humo ambapo Yanga itarejea Jumapili baada ya mchezo huo.
Wachezaji wanaitarajiwa kuondoka kesho ni Ally Mustafa ‘Barthez,’ Deo Munish ‘Dida, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondani, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Salum Telela, Dilunga, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa, Simon Msuva,Amissi Tambwe, Kpah Sherman na Danny Mrwanda

0 maoni:

Post a Comment