Mreno Cristiano Ronaldo
ni staa wa soka Duniani ambaye kutokana na ubora wake mara nyingi
kwenye kurasa za story za michezo huwa zinaandika kuhusu yeye.
Neema imeendelea kubaki upande wake, siku chache zilizopita ameongoza kikosi cha Real Madrid kwenye ushindi mzuri walioupata, goli 2-0 ambapo walikuwa wakicheza na timu ya Elche, leo Christiano Ronaldo anaingia kwenye taarifa nyingine ya kuwa staa ambaye anashika nafasi ya tatu kwa kuifungia timu ya Real Madrid magoli mengi zaidi katika historia ya soka la Hispania na timu yake pia.
Katika mchezo wa juzi Jumapili Ronaldo alihitimisha ushindi wao kwa kufunga goli la pili na kumfanya kufikisha jumla ya magoli 290.
Ronaldo ambaye pia mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or
ya mchezaji bora wa kiume wa mpira wa miguu kwa mara ya tatu ameshika
nafasi hiyo akiwa amecheza michezo 289 huku nafasi ya pili ikishikwa na Alfredo Di Stefano ambaye alicheza michezo 392 na kuwa na magoli 307 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Raul Gonzalez mwenye magoli 323 katika michezo 741.
0 maoni:
Post a Comment