Feb 18, 2015

ALIYE TEMWA SIMBA APATA TIMU RWANDA


Kiungo wa zamani wa Simba, Mrundi, Pierre Kwizera, amebamba dili baada ya kufanikiwa kujiunga na timu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda.

Kiungo huyo ambaye aliichezea Simba kabla ya kufungashiwa virago sambamba na ‘ndugu yake’, Amissi Tambwe, amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu, lakini kama uwezo wake ‘utawakuna’ mabosi wake, ataongezewa mkataba.
Akizungumza kutoka jijini Kigali, Rwanda, kiungo huyo alisema kuwa anafurahia maisha mapya ndani ya klabu hiyo inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Ninamshukuru Mungu nimepata timu, nipo na Rayon Sports ya Kigali. Wamenipokea vizuri na ninafurahi kuwa hapa, wikiendi walikuwa Cameroon kucheza mashindano ya Caf.

“Simba bado hawajanilipa fedha zangu mpaka sasa, lakini akili yangu kwanza ninaielekeza katika kuisaidia timu yangu mpya, baadaye ndiyo nitaanza kufuatilia kuhusu malipo yangu,” alieleza Kwizera ambaye alikuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Ivory Coast msimu wa 2013/2014.

0 maoni:

Post a Comment