Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid
Carlo Ancelotti anaamini mchezaji nyota Christiano Ronaldo ataimarika
punde tu atakapopata bao.
Mchezaji huyo wa Ureno hajafunga katika
mechi zake tatu zilizopita ,na hivyobasi kuzua utata kuhusu kiwango cha
mchezo wake kabla ya mechi ya kilabu bingwa Ulaya dhidi ya Schalke.Ronaldo amekuwa akiugua jeraha la mguu,lakini kocha Ancelotti hana wasiwasi.
''Itakuwa fursa kwa yeye kupata bao wakati wa mechi dhidi ya Schalke'',alisema.
Ni kipindi cha mda mrefu kwa Ronaldo kucheza bila kufunga msimu huu licha ya yeye kupata mabao 38 katika mechi 35.
0 maoni:
Post a Comment