KIUNGO Paul Pogba ameshauriwa na Nicolas Anelka kuhamia Chelsea au Real Madrid ikiwa ataondoka Juventus mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 21 amesaini Mkataba mpya wa mshahara wa Pauni
70,000 kwa wiki na vigogo hao wa Serie A Oktoba mwaka jana ambao
utamalizika Juni 2019.
Lakini taarifa zinasema kwamba, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Pogba anataka kuondoka.
Kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba anatakiwa na klabu kubwa mbalimbali Ulaya
Nicolas Anelka (kulia) akishangilia na Didier Drogba baada ya kuifungia Chelsea dhidi ya Burnley Agosti mwaka 2009
Na
mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Anelka, ambaye
alicheza pamoja na Pogba katika mkopo wake wa miezi mitano Juventus
mwaka 2013, anaamini kwamba Mfaransa huyo anapaswa kwenda Stamford
Bridge au Santiago Bernabeu, kuliko kurejea Manchester United ambako
alikaa kwa miaka mitatu.
"Mtazamo
wangu ni Chelsea, ambao hakika wana wachezaji wakubwa na nguvu ya
kifedha ya [Roman] Abramovich au Real Madrid, ambao ni moja ya klabu
kubwa duniani - ikiwa si kubwa kabisa.
"Na
ninaweza kuona yeye anafanya vizuri huko, pamoja na staili yake ya
uchezaji na kocha wa huko, Carlo Ancelotti atapata mengi kutoka kwake.
Kichwani mwake, Paul atakuwa tayari anafahamu klabu anayotaka kuchezea,"amesema Anelka.
0 maoni:
Post a Comment